Ikiwa ni dakika chache tu baada ya kutangazwa Davido kuwa mshindi wa
tuzo aliyokuwa akiiwania Diamond pia, Diamond amechukua muda wake na
kuandika maneno haya kwa watanzania na wote wanao toa sapoti kwake
Tuesday, July 1, 2014
Trending tonight: Comment ya Ray C kumtaka Tid kuongea nae yamcharua Myama..................
Kikubwa kinachoendelea usiku huu, ni majibu aliyoyatoa TID kwa msanii
mwenzake na mwanaharakati katika kukomesha matumizi ya madawa ya kulevya
Ray C.
Ingawa haijajulikana rasmi ni nini kilicho muudhi Mzee Warioba a.k.a
TID, katika comment aliyoiandika Ray C katika moja ya picha zake
alizozituma Instagram
"Come lets talk Tid ur the best musician in east Africa pls lets talk"
TID alionekana kukerwa na Comment hiyo na kumpa makavu Ray C kwa kumtusi right under her comment
Labels:
BURUDANI
Mwalimu aliyeshinda milioni 3 kwa kutabiri Suarez kumng’ata mtu.............................
Mwalimu mmoja kutoka Sweden ambaye ni shabiki wa mpira ameshinda zaidi ya shilingi milioni tatu za kitanzania baada ya kuweka dau kutabiri kuwa Luis Suarez atamng’ata mtu wakati wa mechi za Kombe la dunia.
Mwalimu huyo Jonathan Brack, 23 kutoka Stenungsund, alitabiri kuwa mchezaji huyo wa Uruguay atamng’ata mpinzani wake wakati wa mechi.
Jonathan amesema kuwa alikuwa akitafuta kitu cha kutabiri kabla ya mechi hiyo na baadae kuona aweke dau juu ya kitendo hicho ambapo rafiki yake alimwambia asipoteze hela yake kwa kitu cha kijinga kama hicho
Jonathan anasema anapanga kutumia pesa hizo kwa ajili ya kuzunguka Uingereza kuangalia mechi za Kombe la dunia ambapo wakati anatabiri alikuwa akiangalia mechi hiyo kati ya Italia na Uruguay mitaa ya nyumbani kwao.
Mrembo aliyeteuliwa kuigiza maisha ya marehemu Aaliyah aikacha dili yenyewe...................
Staa wa Disney channel Zendaya Coleman ameitosa dili ya kuigiza filamu ya maisha ya marehemu Aaliyah ambaye alikuwa nyota wa muziki wa R&B wa nchini Marekani aliyefariki dunia katika ajali ya ndege mwaka 2001.
Mwakilishi wa mwigizaji huyo amesema kuwa nyota huyo hatashiriki tena kama Starring au mwigizaji mkuu wa filamu hiyo.
Kampuni inayotengeneza filamu hiyo ya Lifetime, imesema mipango ya kuanza kuitengeneza filamu hiyo imesubirishwa kwa muda.
Imeripotiwa kuwa baba mdogo wa mwanamuziki Aaliyah ambaye pia alikuwa meneja wake hakutaarifiwa juu ya filamu hiyo.
Hivi ndivyo trend ya #Suarezing ilivyokuwa kubwa mtandaoni................
Baada ya kumng’ata mchezaji mwenzake, Luis Suarez amegeuka kuwa mchezaji anayetrend sana au anayezungumziwa sana kupitia mtandao wa Twitter kwa kutumia hashtag ya #Suarezing huku ikiambatana na picha mbalimbali zilizotengenezwa za kumtania mchezaji huyo kwa kitendo alichofanya.
Tangu mchezaji huyo wa Uruguay apewe adhabu ya kufungiwa kwa kumng’ata mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini amekuwa akimake headlines kila kukicha katika mitandao haswa Twitter.
Ilianza kama utani tu kwa watu kutengeneza picha lakini sasa kimegeuka kuwa kitu kikubwa huku wengine wakijipiga picha hata barabarani kuiga kitendo kilichofanywa na Suarez wakati wa moja ya mechi za kombe la dunia.
Labels:
BURUDANI
Taarifa ya rapa DNA kuondoka Grand Pa Records......................
Mtandao wa Ghafla Kenya umeripoti kuwa, baada ya kudumu na Lebo yake kubwa ya muziki Kenya, Grand Pa Records Rapa DNA ameamua kumaliza mkataba na lebo hiyo na kuamua kuchukua njia yake.
Katika taarifa yao kupitia vyombo vya habari, Grand Pa Records wamesema kuwa mkataba wao na mwanamuziki huyo ulimalizika rasmi Mei mwaka huu ambapo pande zote mbili yani wao na DNA hawakuwa na nia ya kuendelea tena kufanya kazi pamoja hivyo kulazimika kutosaini mkataba mwingine.
DNA akiwa pamoja na Record Lebo hiyo alitoa ngoma kali zilizotamba Afrika Mashariki ikiwemo Banjuka ambayo ilimuweka kwenye ramani nzuri hivyo kwa yeye kuondoka na kuacha kufanya kazi na Grand Pa kumeibua hali ya wasiwasi juu ya mustakabali wa muziki wake miongoni mwa mashabiki lakini hawakusita kumtakia mema aendako.
Hii ni listi mpya ya Forbes ya most powerful celebrities na pesa walizoingiza kwa mwaka.................
Forbes mtandao unaoaminika kwa kutoa list mbalimbali za uhakika hivi sasa wametoa list ya most powerful celebrities pamoja na pesa walizoingiza tangu June 2013 hadi June 2014.
Beyonce amefanikiwa kunaa namba moja akimuacha mume wake nafasi tano nyuma ambaye yupo namba 6. Top 10 ina watu maarufu kama LeBron James,Oprah,Rihanna,Jay Z,Katy Perry na wengine,
Hii ndiyo list ya top 10 na pesa walizoingiza kwa muda wa miezi 12
1) Beyonce: $115million
2)LeBron James – $72million
3)Dr. Dre – $620million
4)Oprah Winfrey- $82million
5) Ellen DeGeneres – $70million
6)Jay Z – $60million
7)Floyd Mayweather- $105million
8)Rihanna – $48million
9)Katy Perry- $40million
10)Robert Downey Jnr – $75million.
Note : Hii ni list ya most powerful celebrities na sio most richest celebrities.
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Posts (Atom)



