Social Icons

Pages

Tuesday, July 1, 2014

Mwalimu aliyeshinda milioni 3 kwa kutabiri Suarez kumng’ata mtu.............................


suarez5

Mwalimu mmoja kutoka Sweden ambaye ni shabiki wa mpira ameshinda zaidi ya shilingi milioni tatu za kitanzania baada ya kuweka dau kutabiri kuwa Luis Suarez atamng’ata mtu wakati wa mechi za Kombe la dunia.
Mwalimu huyo Jonathan Brack, 23 kutoka Stenungsund, alitabiri kuwa mchezaji huyo wa Uruguay atamng’ata mpinzani wake wakati wa mechi.

suarez4

Jonathan amesema kuwa alikuwa akitafuta kitu cha kutabiri kabla ya mechi hiyo na baadae kuona aweke dau juu ya kitendo hicho ambapo rafiki yake alimwambia asipoteze hela yake kwa kitu cha kijinga kama hicho
Jonathan anasema anapanga kutumia pesa hizo kwa ajili ya kuzunguka Uingereza kuangalia mechi za Kombe la dunia ambapo wakati anatabiri alikuwa akiangalia mechi hiyo kati ya Italia na Uruguay mitaa ya nyumbani kwao.

No comments:

Post a Comment

 

Sample text

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates