Muziki mzuri hutengenezwa kwa ustadi wa
mchanganyiko wa ala za sauti na mashairi. Sanaa ya utengenezaji muziki
mzuri ni kazi ambayo watayarishaji na wasanii kwa pamoja huifanya wakati
wa utengenezaji wa wimbo. Mara nyingi, wasanii na watayarishaji wa
muziki hutengeneza muziki kutokana na mazingira halisi yanayowazunguka
katika maisha yao binafsi kama vile maisha ya mapenzi, kazi nk.
Otuck William, msanii mpya kwenye maskio ya wapenzi wengi wa muziki
nchini ambaye pia ni Afisa Tabibu, anaelezea namna ambavyo kazi yake ya
utabibu imechangia katika utengenezaji wake wa muziki.
“Siku yangu ya kawaida kwa kiasi kikubwa
naitumia kusikiliza wagonjwa na wateja wengine wanaokuja kwenye kituo
cha afya ninachofanyia kazi. Ni kitu ambacho ninakipenda maana kinanipa
nafasi ya kusaidia jamii. Imekuwa ni ndoto yangu kwa muda mrefu. Lakini
pamoja na kusikiliza matatizo yao ya afya, ukiwa mhudumu wa afya, watu
hukuamini, wengi watakueleza matatizo yao ya ndani sana ambayo pengine
hawawezi kuwaambia hata wapenzi wao, hivyo kuongea nao kila siku
kunanipa nafasi ya kujifunza mengi sana kuhusu watu na Maisha. Muziki
ninaoufanya ni kwa ajili ya watu na Maisha, hivyo yale nijifunzayo kwa
watu niwaonao kila siku, huwa ninajaribu kuyatafsi katika ala za muziki.
Ni namna moja wapo ya kutengeneza kitu ambacho kinawahusu watu moja kwa
moja. Hivyo kinakuwa bora na kizuri…” – Otuck William
Pamoja na kazi nyingi ambazo ziko studio, mwimbaji huyu wa Soul
anafanya vizuri kwenye vituo mbali mbali vya TV na Redio kupitia rekodi
yake iitwayo “Deja Vu” ambayo imetayarishwa na yeye mwenyewe na video
imeongozwa na kutayarishwa na Nikki Dizzo wa Focus Film Tanzania.Kama bado hujapata nafasi ya kuangalia Video hiyo, hii hapa
Lakini pia unaweza kupakua audio ya deja vu kwenye mtandao wa soundcloud.
https://soundcloud.com/otuckwilliam/deja-vu-otuck-william-ft-hance-puff
Instagram & Twitter @Otuck_William
No comments:
Post a Comment