Featured Posts
Thursday, October 1, 2015
Thursday, February 26, 2015
Dear Melanie Bartz
Tunahukuru
kwa barua pepe ya tarehe 17/10/2014 Tunapenda kuomba Samahani kwa kuchelewa
kuijibu mapema kutokana na sababu ya kiafya kuwa mbaya kutokana na ajali ya
pikipiki iliyopelekea kulazwa muhimbili Hospitali ya Taifa na Kufanyia
Operation ya Kichwa ambayo ilidumu kwa miezi mitatu na sasa hali yangu ni nzuri
na Kwa Heshima na Taadhima napenda kuchukua nafasi hii kujibu maswali ya mradi
wa dipensari ya Kijiji cha Tulila kama ifutavyo
1.
Rasimali watu
Kufatua
matofali 30,000 @Tsh 100 *30,000 = 3,000,000
Kupanga
jiko na kuchoma Tsh 1,500,000
Kubebelea
tofali kupeleka sehemu ya ujenzi Tsh 1,000,000
Kupasua
mawe na kokoto Tunaitaji tripu 10 kila
tripu Tsh 30,000 *10 =300,000
Mchanga
Kwa ajili ya ujenzi kila tripu Tsh 80,000 *10 = 800,000
Kununua
Ramani ya dispenary Tsh 500,000
Kununua
Kiwaanja cha ujenzi wa dispensary Tsh 1,000,000
Tunaitaji
majengo madogo matatu
Ø
Maabara
Ø
Utawala
Chakula na Usafiri Tsh 1,500,000
Emergency cost Tsh 1,400,000
Total cost of Euro 5000 € = Tsh
11,000,000/=
2.
Shughuli za uendeshaji wa dispensary utatokana na gharama za uchangiaji wa
matibabu yatakayo tolewa
3.
Dawa zitapatikana kutokana na fedha za uchangiaji ili kununulia dawa kwenye
maduka ya dawa ya jumla yalioko Wilayani
Yours faithfully
Edward Putuka,
Saturday, August 9, 2014
Unaikumbuka ile kesi ya Samsung na Iphone?hiki ndicho kilichoamuliwa kwa kampuni hizo.......
Ile kesi ambayo inahusu Kampuni ya Apple na Samsung kwa sasa zimekubaliana kuachana na kutupilia mbali kesi zote zilizofunguliwa Marekani zikiwa zimeshitakiana,Kampuni hizo zilizozana kuhusu uanzilishi wa vifaa vya kielektroniki katika nchi kadhaa ikiwemo Uingereza, Korea ya kusini,Japan na Ujerimani.
Kampuni zote mbili zilikuwa zimewasilisha mashitaka mahakamani lakini katika taarifa yao ya makubaliano ya hivi karibuni,kampuni zote mbili zimesema mzozo huo haukua na jambo lolote linalohusiana na leseni na hivyo basi zitaondoa kesi hizo Marekani.
Mwafaka huu kati ya kampuni hizo mbili umeafikiwa baada ya miaka kadhaa ya migogoro ambapo Migogoro yao ilianza mwaka 2011 baada ya Apple kuishtaki Samsung huko Marekani na kudai kuwa kampuni ya Galaxy iliyoko Kusini mwa Korea ilitumia miundo ya iPhone na iPad.
Kampuni ya Galaxy ilijibu mashtaka ya Apple na kuishtaki kwa misingi ya kuingilia haki zake za uanzilishi wa programu za picha,muziki, na picha za video, na pia jinsi ya kunasa na kutuma picha za video mtandaoni.
Apple pia iliwasilisha mashtaka ya kupinga madai ya uanzilishi na Galaxy lakini hatimaye kuafikiana kutupilia mbali kesi hizo za uanzilishi,Apple ilishinda kesi mbili dhidi ya Samsung miaka michache iliyopita.
Mwezi Mei, mahakama moja ya Marekani iliamuru Samsung kulipa dola million 119.6 kwa Apple kwa kuingilia haki zake za uanzilishi. Apple ilikuwa imewasilisha ombi kulipwa dola milioni 2.2.
Vile vile, mahakama hiyo ilikataa kauli kuwa Apple iliingilia haki Fulani za Uanzilishi wa Samsung na kulipa Samsung dola 158,000.
Hata hivyo Samsung ilikana mashtaka hayo na kutaka kulipwa dola milioni 6 kwa madai kuwa Apple ilingilia haki zake za Uanzilishi wa simu Fulani za kisasa zinazoweza kunasa na kupeperusha picha za video
Miaka miwili iliyopita, baraza lingine la waamuzi liliamuru Samsung kulipa Apple dola bilioni 1.05 kwa kutumia maarifa ya Apple kutengeneza vifaa vyao, kinyume na sheria.
Alichokisema Anti Ezekiel baada ya kusemekana anatoka na dansa wa Diamond Platnumz.......................
Mwanzoni mwa wiki hii miongoni mwa stori ambazo zilitoka na kuenea kwenye magazeti kadhaa ni pamoja na inayomhusu Anti Ezekiel kusemekana kuwa anatoka na dansa wa Diamond Platnumz.
Taarifa ya awali ilidai kuwa mpenzi huyo wa dansa wa Diamond alienda kufanya vurugu nyumbani kwa Anti Ezekiel,Anti Ezekiel kapatikana na kaongelea mahusiano yake na Moses Iyobo ambaye ndiye dansa wa Diamond Platnumz.
Huyu ndiye Super Nyota Divaz kwa Mkoa wa Mwanza........................
Mwanza hatimae wametoa Super Nyota wao ambaye amepatikana leo August 07 kwenye viwanja vya Jembe ni Jembe ambapo mshindi aliyeibuka ni Honeya ambae kwa aina yake ya ushiriki usingeweza kuamini kama atashinda.
Miongoni mwa vitu ambavyo vimesemwa na mtoa fomu hizo kuwa msichana huyo kwanza alichelewa kuchukua fomu na kujaza na lingine ambalo limewashangaza hata majaji ni pale alipokuja tayari wenzake wameanza lakini kwa alichokifanya hakuna mtu aliyeamini.
Nakumbuka Fetty ambaye ndiye alikua Jaji mkuu alimuuliza kama aliwahi kuimba sehemu yoyote ambaye inamfanya kujua kupangilia muziki wake kama muziki wa bendi lakini msichana huyo alisema hajawahi ingawa ana single aliwahi kurekodi.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa asubuhi ya leo August 07.
Subscribe to:
Comments (Atom)