Social Icons

Pages

Tuesday, July 1, 2014

Taarifa ya rapa DNA kuondoka Grand Pa Records......................


dna1

Mtandao wa Ghafla Kenya umeripoti kuwa, baada ya kudumu na Lebo yake kubwa ya muziki Kenya, Grand Pa Records Rapa DNA ameamua kumaliza mkataba na lebo hiyo na kuamua kuchukua njia yake.
Katika taarifa yao kupitia vyombo vya habari, Grand Pa Records wamesema kuwa mkataba wao na mwanamuziki huyo ulimalizika rasmi Mei mwaka huu ambapo pande zote mbili yani wao na DNA hawakuwa na nia ya kuendelea tena kufanya kazi pamoja hivyo kulazimika kutosaini mkataba mwingine.

dna

DNA akiwa pamoja na Record Lebo hiyo alitoa ngoma kali zilizotamba Afrika Mashariki ikiwemo Banjuka ambayo ilimuweka kwenye ramani nzuri hivyo kwa yeye kuondoka na kuacha kufanya kazi na Grand Pa kumeibua hali ya wasiwasi juu ya mustakabali wa muziki wake miongoni mwa mashabiki lakini hawakusita kumtakia mema aendako.

Hii ni listi mpya ya Forbes ya most powerful celebrities na pesa walizoingiza kwa mwaka.................



bey

Forbes mtandao unaoaminika kwa kutoa list mbalimbali za uhakika hivi sasa wametoa list ya most powerful celebrities pamoja na pesa walizoingiza tangu June 2013 hadi June 2014.
Beyonce amefanikiwa kunaa namba moja akimuacha mume wake nafasi tano nyuma ambaye yupo namba 6. Top 10 ina watu maarufu kama LeBron James,Oprah,Rihanna,Jay Z,Katy Perry na wengine,
Hii ndiyo list ya top 10 na pesa walizoingiza kwa muda wa miezi 12

1) Beyonce: $115million
 2)LeBron James – $72million
 3)Dr. Dre – $620million
4)Oprah Winfrey- $82million
5) Ellen DeGeneres – $70million
6)Jay Z – $60million
7)Floyd Mayweather- $105million
8)Rihanna – $48million
9)Katy Perry- $40million
10)Robert Downey Jnr – $75million.
Note : Hii ni list ya most powerful celebrities na sio most richest celebrities.

Hiki ndicho kiasi kilichotumika kuikamilisha video ya wimbo wa Kerewa wa Shettah.


shetah2

Muziki wa Tanzania kwa sasa umetoa ajira kwa vijana wengi ambao baadhi yao wameamua kuwekeza kwa hali na mali,katika list ya vijana wanamuziki wa Tanzania ni pamoja na Shettah ambaye singo yake ya Kerewa ameenda kufanyia video yake South Africa.

shettah3

Kupitia exclusive interview na millardayo.com Shettah amekubali kutaja kiasi kilichotumika ili kuikamilisha video ya Kerewa>>’Video ya Kerewa ukitoa gharama gharama zingine imenigharimu kama Milion 25 za Kitanzania’

shetah3

‘Yeah Kwa sababu Director God Father peke ake kachukua Milion 19 kuna ndege zile,kukaa,chakula ingawa Dstv pia wameongeza mtonyo lakini kitu kikubwa ni hotel kwa sababu kwa siku tulikua tunalipa pesa za Kitanzania kama 450,000 hivi’
‘Hotel nimeanza kukaa Cape Town nikaenda kukaa Durban baadae Johannesburg yaani hotel pekeake nimetumia zaidi ya Milion 3 za Kitanzania,nina furaha kile nilichoenda kukitafuta nimekipata’.

Alichopost Luis Suarez akiomba msamaha – Chiellini amjibu
















Siku kadhaa baada ya kufanya kitendo cha kumng’ata mchezaji Giorgio Chiellini katika mchezo wa hatua ya makundi kati ya Uruguay vs Italy, na kuadhibiwa kifungo cha miezi minne nje ya soka, hatimaye jana usiku Luis Suarez aliamua kufanya kitendo ambacho wengi hawakukitegemea.
Akitumia akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Luis Suarez aliandika ujumbe mfupi akiomba msamaha kwa Giorgio Chiellini na wanafamilia wa soka ulimwenguni kote kutokana na kitendo alichofanya.
Suarez ambaye aliadhibiwa kifungo cha mechi tisa zinazosimamiwa na FIFA pamoja na kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miezi 4, amekiri makosa yake na kuahaidi tukio kama lile halitojirudia tena.

suarez copy

Muda mfupi baada ya Suarez kutuma ujumbe huo – Chiellini alimjibu na kumwambia amemsamehe na angependa FIFA impunguzie adhabu.

MILLARD AYO ANG'AA KATIKA TUZO ZA WATU, NA HAYA NDO MANENO YAKE BAADA YA KUTWAA TUZO HIZO .........

 
Millard Ayo
 
Na haya ndo maneno yake>>>> Watu wangu!! kwanza namshukuru Mungu muweza wa yote... shukrani kubwa zinazofata ni zako mtu wangu ulienipigia kura, uliefanya kampeni kwenye page yako na kunitag na hata ulieshindwa kupiga kura lakini love yako ilikua kwangu! nyinyi ndio mmeifanya # June272014 kuwa siku yangu nyingine kubwa baada ya kushinda tuzo zote mbili nilizokua nawania ktk # tuzozawatu2014 # MtangazajiAnaependwa na # kipindicharediokinachopendwa asanteni yani watu wangu! Huu ni Upendo mkubwa sana kwangu! ahadi yangu ni ileile # damdam # milele mtu wako wa nguvu na watu wake wa nguvu! Love kwa watu wangu @bdozen na Maryam Kitosi tuliokua pamoja kwenye kuwania, naitambua kazi yenu watu wangu.

MTOTO WA MIAKA 13 AIOKOA NIGERIA ISILIPULIWE BOMU




Siku chache baada ya kutokea shambulizi kubwa la bomu katika soko kubwa ‘Mall’ jijini Abuja, Nigeria mtoto mwenye umri wa miaka 13 amesaidia kuwaokoa raia wa Nigeria kushambuliwa na bomu kubwa baada ya kulishitukia na kutoa taarifa polisi. Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa Kano, aliyejitambulisha kwa jina la Magaji Majiya, mtoto huyo wa kiume alipata mashaka baada ya kuona gari fulani bovubovu likiwa limetelekezwa huku likiwa na mzigo mkubwa karibu na msikiti mmoja. Na ndipo alipolichungulia kuona vitu kama mabomu na akatoa taarifa mapema. “Bomu liliwalenga watu walioenda kuabudu katika msikiti huo na lilikuwa limewekwa kwenye gari aina ya Toyota Tercel.” Alisema Majiya. Polisi walituma kikosi maalum cha kutegua mabomu ambacho kilifanikiwa kulitegua bomu hilo. Mtu mmoja amekamatwa kutokana na tukio hilo.

BARUA YA WAZI KUTOKA KWA EMANUEL MBASHA [ MUME WA FROLA MBASHA ] KWENDA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA IKO HAPA




BARUA KUTOKA KWA MUME WA FLORA MBASHA KWENDA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA: "Mchungaji ...yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri' wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwako. Mchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!! Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!! Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini! Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha?? Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo?? Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa! Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!! Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!! Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!! Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!! Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!! Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako... na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!! Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!! Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!! Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu?? Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana! Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!! Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!!  Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!! Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!! Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!! Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!! Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!! Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti! Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!! Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda.
 

Sample text

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates