Social Icons

Pages

Saturday, August 9, 2014

Unaikumbuka ile kesi ya Samsung na Iphone?hiki ndicho kilichoamuliwa kwa kampuni hizo.......


glx

Ile kesi ambayo inahusu Kampuni ya Apple na Samsung kwa sasa zimekubaliana kuachana na kutupilia mbali kesi zote zilizofunguliwa Marekani zikiwa zimeshitakiana,Kampuni hizo zilizozana kuhusu uanzilishi wa vifaa vya kielektroniki katika nchi kadhaa ikiwemo Uingereza, Korea ya kusini,Japan na Ujerimani.
Kampuni zote mbili zilikuwa zimewasilisha mashitaka mahakamani lakini katika taarifa yao ya makubaliano ya hivi karibuni,kampuni zote mbili zimesema mzozo huo haukua na jambo lolote linalohusiana na leseni na hivyo basi zitaondoa kesi hizo Marekani.
Mwafaka huu kati ya kampuni hizo mbili umeafikiwa baada ya miaka kadhaa ya migogoro ambapo Migogoro yao ilianza mwaka 2011 baada ya Apple kuishtaki Samsung huko Marekani na kudai kuwa kampuni ya Galaxy iliyoko Kusini mwa Korea ilitumia miundo ya iPhone na iPad.
Kampuni ya Galaxy ilijibu mashtaka ya Apple na kuishtaki kwa misingi ya kuingilia haki zake za uanzilishi wa programu za picha,muziki, na picha za video, na pia jinsi ya kunasa na kutuma picha za video mtandaoni.
Apple pia iliwasilisha mashtaka ya kupinga madai ya uanzilishi na Galaxy lakini hatimaye kuafikiana kutupilia mbali kesi hizo za uanzilishi,Apple ilishinda kesi mbili dhidi ya Samsung miaka michache iliyopita.
Mwezi Mei, mahakama moja ya Marekani iliamuru Samsung kulipa dola million 119.6 kwa Apple kwa kuingilia haki zake za uanzilishi. Apple ilikuwa imewasilisha ombi kulipwa dola milioni 2.2.
Vile vile, mahakama hiyo ilikataa kauli kuwa Apple iliingilia haki Fulani za Uanzilishi wa Samsung na kulipa Samsung dola 158,000.
Hata hivyo Samsung ilikana mashtaka hayo na kutaka kulipwa dola milioni 6 kwa madai kuwa Apple ilingilia haki zake za Uanzilishi wa simu Fulani za kisasa zinazoweza kunasa na kupeperusha picha za video
Miaka miwili iliyopita, baraza lingine la waamuzi liliamuru Samsung kulipa Apple dola bilioni 1.05 kwa kutumia maarifa ya Apple kutengeneza vifaa vyao, kinyume na sheria.

Baada ya Davido kuongelea beef lao, Wiz Kid amjibu kupitia twitter....................................


kid2

Baada ya jana Davido kuzungumzia kitu gani kilimkasirisha hadi bifu na Wiz Kid kutokea, Wiz ameingia twitter na kumjibu bila kumtaja jina kama kawaida yao. Tweet hiyo inadhihirisha kwamba Wiz Kid hakupenda jinsi Davido alivyozungumza kuhusu hilo beef.

kid

Alichokisema Anti Ezekiel baada ya kusemekana anatoka na dansa wa Diamond Platnumz.......................



anti ezekiel

Mwanzoni mwa wiki hii miongoni mwa stori ambazo zilitoka na kuenea kwenye magazeti kadhaa ni pamoja na inayomhusu Anti Ezekiel kusemekana kuwa anatoka na dansa wa Diamond Platnumz.
Taarifa ya awali ilidai kuwa mpenzi huyo wa dansa wa Diamond alienda kufanya vurugu nyumbani kwa Anti Ezekiel,Anti Ezekiel kapatikana na kaongelea mahusiano yake na Moses Iyobo ambaye ndiye dansa wa Diamond Platnumz.

Huyu ndiye Super Nyota Divaz kwa Mkoa wa Mwanza........................




21dnc

Mwanza hatimae wametoa Super Nyota wao ambaye amepatikana leo August 07 kwenye viwanja vya Jembe ni Jembe ambapo mshindi aliyeibuka ni Honeya ambae kwa aina yake ya ushiriki usingeweza kuamini kama atashinda.
Miongoni mwa vitu ambavyo vimesemwa na mtoa fomu hizo kuwa msichana huyo kwanza alichelewa kuchukua fomu na kujaza na lingine ambalo limewashangaza hata majaji ni pale alipokuja tayari wenzake wameanza lakini kwa alichokifanya hakuna mtu aliyeamini.
Nakumbuka Fetty ambaye ndiye alikua Jaji mkuu alimuuliza kama aliwahi kuimba sehemu yoyote ambaye inamfanya kujua kupangilia muziki wake kama muziki wa bendi lakini msichana huyo alisema hajawahi ingawa ana single aliwahi kurekodi.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa asubuhi ya leo August 07.

DSC_0394
DSC_0395
2dnc

13dnc
6dnc
3dnc

22dnc
26dnc
Mshindi wa Super Nyota Divaz Mwanza 2014 Honea akiimba.
35dnc
Baadhi ya washiriki wa Fiesta Super Nyota Divaz Mwanza 2014.
37dnc
39dnc
Muda wa kuwajua tatu bora ulikua huu.
43dnc
79dnc
83dnc
Hawa ni washindi wa nafasi ya kwanza na ya pili.
86dnc

Mshindi wa kwanza wa Super Nyota Divaz Mwanza 2014 Honea
106dnc
110dnc
115dnc

Friday, August 8, 2014

Pichaz za baadhi ya Wasanii waliotua Mwanza tayari kwa ajili ya Serengeti fiesta kesho CCM Kirumba.................


59prss

Baada ya kupatikana kwa mshindi wa Super Nyota na washindi wa Dance la Fiesta ambao wote walipatikana jana kwenye ukumbi wa Jembe ni Jembe Beach Resort leo wasanii mbalimbali wameongea na waandishi wa habari.
Wasanii hao ni wale ambao wataperfoam kesho waliofika ni pamoja na Ney wa Mitego,Young D,Mr.blue,Barakah Da Prince,Chegge na Temba,Madee,Makomando,Stamina,Young Killer,Vanessa Mdee na wengine kibao.
Miongoni mwa wasemaji wa mkutano huu na waandishi wa habari ni pamoja na Mwenyekiti wa shamrashamara za Serengeti Fiesta Sebastian Maganga ambaye amesema kuwa sababu ya kuanza kwa Serengeti Fiesta kwa mkoa wa mwanza ni kama watu wana kumbukumbu mwaka 2004 Serengeti Fiesta ya kwanza kutoka nje ya Dar ilikua ni ndani ya jiji la Dar ambayo ilikua na kauli mbiu ya Utamaduni unaendelea.
Kwa miaka 10 hii kwa sasa wameweza kushuhudia namna ilivyosambaza upendo ambayo imewajumuisha wasanii wadogo na wakubwa na safari hii Serengeti fiesta imeongeza miji na itakuwa miji 18 badala ya 14 ya mwaka jana.
Hizi ni baadhi ya picha za mkutano huo.
 
1prss


2prss
3prss
4prss
6prss
7prss
5prss
11prss
12prss
13prss
14prss
15prss
16prss
17prss
18prss
28prss
29prss
30prss
33prss
46prss
43prss
42prss
38prss
37prss
36prss
47prss
49prss
58prss
59prss
61prss
66prss
77prss
75prss
74prss
73prss
68prss
67prss
78prss
80prss
82prss
83prss
89prss

 

Sample text

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates