Social Icons

Pages

Monday, June 30, 2014

BIOGRAPHY: MUFIED MOHAMMED HAMAD (Director, Producer & Photographer)


1982025_10201596157133466_1221728513_n
MUFIED MOHAMMED HAMAD
DIRECTOR , PRODUCER & PHOTOGRAPHER
FIDDZ PRODUCTIONS.
If ambition and hard work is your motto in life, then meet Mufied Hamad a young and talented man who has always been chasing his dreams since he was a young boy. Born in 1988 in a small town of Shinyanga in Tanzania, Mufied completed his High school education at Lenana School in Nairobi Kenya. He then worked as an Account Executive at Techno Brain in Dar-es-Salaam before he travelled to USA in Jan 2010 to get his Bachelor’s Degree in business Administration/Management at Arkansas State University.
With the right exposure and resources Mufied got the opportunity to further his skills and child hood ambition to become a film director and photographer. He is currently working with local artists to produce music videos and is also working on his own movie projects such as “Magdalene” a suspenseful drama, and a breath taking thriller “Revenge” which will be coming out soon. Mufied hopes to start his own production company and also grow his photography business in Tanzania once he completes his studies.

BIOGRAPHY: PROF JAY (@Profesa_Jay)


3308_92724411494_5407156_n
Joseph Haule (amezaliwa tar. 29 Desemba1975) ni msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Professor Jay. Katika Tanzania, Prof. Jay anatazamika kama msanii aliyeweza kuwateka wazee waweze kusikiliza muziki wa Bongo Flava. Hasa kwa kibao alichofanya wakati yupo na kundi la Hard Blasters Crew – Chemsha Bongo. Professor Jay anatokea kundi la Hard Blasters Crew. Kundi hili ni moja ya makundi yaliyofanya muziki huu ambao hujulikana kama ‘muziki wa kizazi kipya’ kukubaliwa na sehemu kubwa ya wa Tanzania.
Maisha ya muziki
Professor Jay alianza shughuli za muziki mnamo miaka ya 90 hivi na alijiunga na kundi la ‘Hard Blasters Crew‘(HBC) mnamo mwaka 1994. Mwaka 1995 Jay na HBC walishinda kuwa kundi bora la Hip Hop nchini Tanzania. Jay na HBC walitoa albamu ya kwanza iitwayo ‘Funaga Kazi’ mwaka 2000 Albamu hiyo inaaminika kwamba ilileta mapinduzi makubwa sana ya muziki wa Hip Hop nchini Tanzania. Albamu hii yenye ujumbe mzito ina nyimbo kama ‘Chemsha Bongo’ na ‘Mamsapu’ ambazo zilichangia kufanya muziki wa ‘Bongo Flava‘ kuwa wa kila rika na kupewa heshima. Kabla ya hapo muziki huu ulionekana kuwa ni muziki wa wahuni
3308_92724396494_2091701_n

Msanii Binafsi

Professor Jay aliamua kuwa msanii binafsi mnamo 2001 na muda mfupi baada ya hapo akatoa albamu yake ya kwanza iitwayo “Machozi Jasho na Damu”. Albamu hii ilivuma haraka sana na kumfanya Prof. Jay kupata tuzo ya kuwa mtunzi bora wa Hip Hop nchini Tanzania kwa nyimbo yake ya ‘Ndio Mzee’ kutoka kwenye albamu hiyo. na ikifuatiwa na Nyimbo ya “Piga Makofi na Bongo Dar es Salaam
Mwaka 2003 Alitoa albamu ya pili iitwayo “Mapinduzi Halisi” ambayo nayo ilishinda tuzo ya Kili Music Awards kuwa albamu bora ya Muziki wa Hip Hop nchini Tanzania kwa mwaka 2003. Albamu hii imebebanNyimbo kama “Zali la Mentali”, “Msinitenge,” na “Promota Anabeep”
Mwaka 2006 Januari alitoa albamu ya tatu iliyoitwa “J.O.S.EP.P.H”. Jina la albamu hii lilitokana na nyimbo iliyotoka Mwanzo kabla ya Albamu kutoka. Nyimbo hii ilichaguliwa kuwa nyimbo bora ya Bongo Flava kwenye BBC na Radio One Awards.
Mpya imewahi kuteuliwa kuwa ni albamu bora ya Hip Hop , Mtunzi bora wa nyimbo za Hip Hop, na Nyimbo bora ya Hip Hop ya mwaka kwenye Kili Music Awards. 2006.”Nikusaidieje”. na Baadae Kisima Music Awards ya Kenya ilikuwa Nyimbo bora ya Hip Hop na Video bora ya Hip Hop kutoka nchini Tanzania.
3308_92724446494_6157945_n

Albamu

3308_92724456494_3143409_n

Tuzo Alizopata

Wasanii alioshirikiana nao kimuziki

Lady Jay Dee. ( Bongo Dar es Salaam na Nimeamini)
Mc Babu Ayubu. ( Ndio Mzee )
Juma Nature. ( Ndio Mzee na Zali la Mentali )
Q Chilah. ( Msinitenge )
Inspector Haroun. ( Hakuna Noma )
Simple X. ( Piga Makofi na Hakuna Noma )
Jose Chameleone. ( Ndivyo Sivyo – Kutoka Uganda )
Adili a.k.a Hisabati

Mwana FA (ni jukumu letu)

Albert magweir (Una)

Lady Jay Dee (Bongo Dar es Salaam & Niamini )

Mr II sugu (Inatosha)

Ngoni (Mapinduzi)

Jay Mo (Tathimini)

Ferooz (Zubeda)

Mkoloni (Promota anibeep) nk.

Diamond Plutnum (Kipi sijasikia)

Picha za utengenezaji wa video mpya ya KALA JEREMIAH feat NAY WA MITEGO & MO MUSIC “SIMU YA MWISHO” Picha ziko hapa


IMG_3280
Hizi ni picha za utengenezaji wa video mpya ya Kala Jeremiah akiwa nandugu zake kama Nay wa Mitego pamoja na Mo Music, wimbo unaitwa SIMU YA MWISHO ikiwa imetengenezwa na Prod Mona Gangsta na video yake imesimamiwa na Pablo kutoka D360
IMG_3281 IMG_3282 IMG_3283 IMG_3284 IMG_3285 IMG_3286 IMG_3287

Mwanamuziki Msami akiri kuwa mpenzi wa Uwoya, azungumzia tofauti ya umri na mipango yao


Mwanamuziki Msami akiri kuwa mpenzi wa Uwoya, azungumzia tofauti ya umri na mipango yao
Mkali wa Sound Track ambaye pia ni mkali wa kuvunja (dancer) amezungumzia uhusiano wake na muigizaji mrembo wa Bongo Movies, Irene Uwoya.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Msami alizunguka sana mbuyu kutaka kutoa maelezo kuhusu ukweli wa mambo kati ya wawili hao lakini kwa mara ya kwanza aliamua kuiambia tovuti ya Times Fm kauli yake kutokana na jinsi alivyoulizwa.
“Kaongea kwa upole huyu jamaa, kaapproach ili apate jibu. Ni kweli (kicheko)…nimekuridhisha lakini, nimeamua kukuridhisha.” Amesema Msami..
Muonekano wa Irene Uwoya na Msami kwa muonekano uliwafanya wengi wazungumze kwenye mitandao ya kijamii kuwa Msami amegeuka Serengeti Boy kwa Uwoya ambaye wanaamini anamzidi sana umri. Lakini ukweli ni kwamba Msami ni mkubwa kwa Uwoya. Chukua hiyo!
“Unajua mimi mwanzo, Serengeti Boy nilikuwa sina tafsiri yake kabisa yaani. Yaani ile deeply nilikuwa sina tafsiri yake kabisa yaani. Kwa hiyo leo ndio nimepata tafsiri yake ‘Serengeti Boy’ kumbe ni mtu ambaye amezidiwa umri. Tofauti na mimi nilivyokuwa nawaza kuhusu Serengeti Boy.
“Lakini mbona nikasema kama ni hivyo, as we are best friends lakini (joke), lakini mbona mimi nimemzidi umri Uwoya. Lakini mimi ni mkubwa kwake sema yeye ananizidi umri. Mimi ni mkubwa kwake nimemzidi miezi mingi…yaani wewe jua nimemzidi miezi mingi. Mimi ni mkubwa kwa Uwoya.” Alisisitiza Msami 
Katika hatua nyingine, Msami ameeleza mpango wake na Uwoya kutoa filamu ya pamoja na jinsi filamu itakavyokuwa.
Amesema katika filamu hiyo yeye ndiye mhusika kuu na kwamba ni filamu ambayo itahusisha dance na muziki. Filamu hiyo itatoka mwaka huu lakini bado haijapata jina rasmi na tarehe ya kutoka.
“Movie inakuja very soon, watu wakae tayari.” Amesisitiza.
21.06.2014 -  Tags:  msami  uwoya 

SHEHE Amcharukia Jackline Wolper. Ni kutokana na tabia yake ya kubadili badili dini...............


SHEHE Amcharukia Jackline Wolper. Ni kutokana na tabia yake ya kubadili badili dini.
TABIA ya staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper kubadilibadili dini mara kwa mara imeonekana kuwakera watu mbalimbali akiwemo Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum ambaye amemcharukia vikali.

Wolper kiimani ni Mkristo lakini hivi karibuni alibadili na kuwa Muislam kabla ya kurejea tena kwenye imani yake ya awali ya ukristo.

Sababu ya Wolper kubadili dini ilikuwa ni kufunga ndoa na aliyekuwa mchumba wake Abdallah Mtoro ‘Dalas’, walipoachana akaamua kurudi kwenye ukristo.

Akizungumza na Risasi Jumamosi juzikati, Shehe Salum, alisema Wolper anapaswa kujichunguza na kubadilika haraka kwani kitendo anachofanya ni kinyume na taratibu za dini.
“Siyo vizuri hata kidogo na hata dini zote zinakemea kitendo cha kuchezeachezea dini kwani ni chukizo kwa Mungu.

“Kwa upande wa Dini ya Kiislamu, kuna sheria kali zaidi kwa mtu akionekana na tabia hiyo, anaweza hata kuuawa hivyo wanaofanya mchezo huo waache kwani siyo vizuri. Huko ni kumfanyia Mungu dhihaka,” alisema Shehe Salum na kuongeza:

“Unajua suala la imani ni kitu kinachomhusu mtu binafsi, ni vyema kufanya uamuzi wa hakika na kushika njia moja na siyo kufanya dhihaka na dini ya Mwenyezi Mungu. Ni kitu kibaya sana.”
Naye Juma Suleiman, mkazi wa Ilala, jijini Dar es Salaam alimwambia mwandishi wetu kuwa, katika imani ya kiislam kunakatazwa watu kucheza na dini huku akisisitiza anayefanya hivyo anaweza kulaaniwa.

Wema na kajala wamaliza tofauti zao.


Wema na kajala wamaliza tofauti zao.

Habari mpya kama sio njema ni kuwa Wema Sepetu na Kajala Masanja wamemaliza tofauti zao zilizotokana na ‘beef’ lao lilichukua week kibao sasa. Kwa mujibu wa taarifa mpya mitandaoni ni kuwa mastaa hao wawili ambao waliwahi kuwa mashosti wakubwa walimaliza ‘beef’ lao katika sherehe ya kibao kata cha mwandishi wa magazeti ya Globalpublishers anayeitwa Imelda Mtema.

 Katika tukio hilo mastaa kibao walihudhuria akiwemo Aunty Ezekiel ambaye kwasasa amekuwa karibu zaidi na Wema Sepetu. Nae Wema Sepetu kupitia Instagram ame-share picha hiyo hapo juu akiwa na kina Kajala na kuandika "nawapenda sana hawa hapa..jana hiyo kwa kibaokata cha Imelda Mtema"

PHOTO’S: Yaliyojiri Sunday Family POOL PARTY @ Escape 2


IMG_7168 IMG_7177 IMG_7179 IMG_7190 IMG_7207 IMG_7211 IMG_7215 IMG_7216 IMG_7220 IMG_7228 IMG_7231 IMG_7253 IMG_7257 IMG_7263 IMG_7285 IMG_7311 IMG_7314 IMG_7316 IMG_7326 IMG_7328 IMG_7333 IMG_7343 IMG_7348 IMG_7373 IMG_7411 IMG_7429 IMG_7469 IMG_7484 IMG_7536 IMG_7543 IMG_7551 IMG_7557 IMG_7562 IMG_7575 IMG_7580 IMG_7582
Kila Jumapili Escape 2 inakuletea Family Pool Party kwa kiingilio cha elfu 7 kwa wakubwa na elfu 3 kwa watoto

 

Sample text

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates